CAF imetangaza kuitoa ES Setif Ligi ya Mabingwa Afrika
June 24 2016 shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza maamuzi magumu ya kuitoa klabu ya ES Setif ya Algeria katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, katika hatua ya nane bora hivyo kufanya Kundi B libaki na timu za Enyimba, Mamelodi Sundowns na Zamalek.
CAF wamefikia maamuzi
hayo baada ya kukaa chini na kupitia vifungu vya sheria, ni adhabu gani
inastahili kwa klabu hiyo, ambayo imetolewa katika mashindano hayo kwa
kosa la mashabiki wake kufanya fujo katika uwanja wao wakati wa mchezo
dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini June 19 2016.
No comments:
Post a Comment