Tangakumekuchablog
Mkinga, WAKAZI
wa kijiji cha Mwanyumba kata ya Bwiti
Tarafa ya Maramba Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, wameitaka Serikali
kurejesha mfumo wa upatikanaji wa maji safi baada ya miundombinu yake kuchakaa.
Wakizungumza na waandishi wa habari
juzi, wakazi hao wamesema hali za afya zao ziko mashakani baada ya kutumia maji
ya mto ambayo pia hutumiwa kwa ajili ya kunyweshea mifugo.
Walisema mbali ya uchakavu huo
unapotokea ujio wa viongozi wa Serikali maji hutoka katika mabomba na kuwapa
mashaka wa upatikanaji wa maji wa kila siku na kuondokana na kupatwa na
magonjwa ya tumbo na kichocho.
“Ajabu hapa tuko na mwaka bomba
halitoi maji lakini ujio wa viongozi wa Serikali imekuwa neema kwetu, tumekuwa
tukitumia maji ya mito ambayo pia hutumiwa na wanyama” alisema Asha Bakary na
kuongeza
“Usikiapo ujio wa viongozi wa
kitaifa ujue maji yatatoka ila tatizo
hatuna vifaa vya kuhifadhia , ila leo ni sikukuu ya wa watu wa Mwanyumba”
alisema
Alisema kuna kitisho cha kuzuka kwa
magonjwa ya tumbo na kichocho baada ya wakazi wote kutumia maji ya mto kwa
matumizi ya kunywa kupikia na kuongea wakiwemo wanyama.
Akizungumzia kero hiyo, Mwenyekiti
wa Serikali ya kijiji kata ya Magati, Kimwaga Shauri, alisema uhaba huo wa maji kijiji cha Mwanyumba
imetokana na vijiji kuongezaka ambapo awali kijiji hicho kilikuwa hakimo katika
mradi wa maji.
Alisema kuongezaka kwa vijiji
imekuwa sababu ya baadhi ya maeneo kukosa maji kwa baadhi wa wakati na kusema
kuwa Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na maji
safi na salama.
“Mradi wakati ulijengwa ulikuwa wa
vijiji vitatu na sasa tuko na vijiji
saba jambo ambalo linatupa wakati mgumu kuyagawa na kuzifkia kaya ikiwemo
kijiji cha Mwanyumba ambacho hakikuwemo katika mradi” alisema Shauri
Alisema jitihada za kuhakikisha maji
yanapatikana kijijini kwa kutumia mfumo wa zamu unafanyika na kuwataka wananchi
kulinda vyanzo vya maji na kuacha kukata miti .
Mwisho
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment