England yapata kocha wa muda
Chama cha soka
nchini England kinajiandaa kumtangaza Gareth Southgate kuwa kocha wa
muda wa timu yake ya taifa katika mwanzo wa kampeni za kuwania kufuzu
kombe ka dunia.
Zoezi la kumsaka kocha mpya litaanza baada ya michezo ya awali ya kufuzu kufanyika.Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzuluMtendaji mkuu wa FA Martin Glenn,amesema kuwa kupatikana kwa kocha mpya kunaweza kuchukua miezi kadhaa,huku pia akimtaja meneja wa Arsenal,Arsene Wenger ambaye anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake kama moja ya chaguo lao.
bbc
No comments:
Post a Comment