Tangakumekuchablog
Tanga, MKUU wa Wilaya
ya Mkinga Tanga, Mboni Mgazza, amesema hatomvumilia mzazi yoyote ambaye mtoto
wake haendi shule na kusema kuwa msako wa kuwasaka nyumba mmoja mmoja
atauanzisha.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya
siku ya mtoto wa Afrika juzi iliyofanyika Kiwilaya kijiji cha Mwanyumba kata ya
Bwiti Tarafa ya Maramba Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, alisema wimbi la watoto
wasioenda shule linaongezeka.
Alisema kuna baadhi ya wazazi
wamekuwa wakiwatumikisha watoto wao kwenye kazi za mifugo na kilimo na kusahau
umuhimu wa kumpatia elimu ambayo itamsaidia katika maisha yake ya mbeleni.
“Leo tunaadhimisha siku ya mtoto wa
Afrika, tumeona changamoto wanazozipata na baadhi yao kunyanyaswa hata na
wazazi wao, hili sitoweza kulivumilia katika Wilaya yangu, alisema Mboni na
kuongeza
“Ofisi yangu itafanya msako wa
nyumba kwa nyumba kuwafichua wazazi
ambao wamewafingia ndani watoto wao na kuwakosesha haki ya msingi ya kupata
elimu’alisema
Akizungumzia manyanyaso ya watoto
wanaopata kutoka kwa baadhi yawatu ikiwemo kuwafungia ndani iwe kwa ulemavu au chuki, Mboni alisema kwake
hatolivumilia na kuitaka jamii kuwafichua watu wenye tabia hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Empower Sociaty Build The Nation (ESBN) ambaye yuko na kituo cha watoto, Poul Devid, aliitaka jamii kuwasaidia watoto wanaolelewa katika vituo vyabkulelea
yatima.
Alisema vituo vingi vya watoto
vinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mahitaji muhimu ya vykula, nguo na
madawa pamoja na miundombinu kwa walemavu.
“Tuko na changamoto nyingi katika
vituo vyetu vya kulea watoto ikiwemo
madawa na mahitaji ya kila siku ya binadamu, tunaomba wenye uwezo kuwasaidia
ili nao kuweza kuishi kama wenzao.
Alisema misaada ambayo wamekuwa
wakipata kutoka kwa baadhi ya watu imekuwa haitoshelezi na kukidhi haja kwa
watoto hivyo ni vyema jamii kuwaangalia kwa jicho la pili.
Mwisho
No comments:
Post a Comment