Wednesday, June 29, 2016

POLISI TANGA YAKAMATA MAJAMBIA, VISU NA BUNDUKI TATU RISASI 23 MAPANGONI AMBONI



Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI La Polisi Mkoani Tanga, limesema limekamata vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vikitumika katika matukio ya uhalifu na mauaji vikiwemo visu na majambia.
Akizungumza waandishi wa habari ofisini kwake laeo, Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Leonard Poul, alisema kukamatwa kwa vifaa hivyo ni ushirikiano na vyombo vya usalama na wananchi.
Alisema kwa sasa Mapango ya Amboni yako salama na hakuna kitisho wala masalia ya majambazi na kusema kuwa asilimia mia Mapango hayo yako katika amani na kuwataka wananchi kufanya kazi zao za kila siku bila woga.
Amesema katika kmsako huo ambao ulifanywa toka kutokea tukio la mauaji Polisi walikuwa wakifanya kazi usiku na mchana na kufanikiwa kukamata bunduki tatu aina ya SMG, risasi 23 na majambia pamoja na mapanga.
                                                      
“Toka kutokea tukio la watu 8 kuchinjwa kikatili na matukio ya kuuwawa watu katika maduka makuba na vituo vya mafuta na  uporaji, polisi walikuwa katika msako mkali na leo hii niseme Mapango ya Amboni ni Salama” alisema Poul na kuongeza
“Kwenye msako huu tumewakamata watu watatu ambao walitupa ushirikiano kwa kutuonyesha silaha walipokuwa wamezificha na kweli tuliona shehena ya silaha zikiwemo bunduku aina ya SMG na Majambia” alisema
Hata hivyo kamanda alisema katika tukio hilo la  Majambazi amedai kuwa kuna watu wanatoa ushirikiano hivyo kusema kuwa wote ambao walikuwa wakiunga mkono mkono wa Polisi utawafika.
Katika operesheni hiyo ambayo polisi ilikuta vyombo na madumu ya maji pamoja na utumbo wa Ng’ombe na Mbuzi ambao walikuwa wakichinja pamoja na vifaa vya kujengea kwa kufanya makazi ya kudumu zikiwemo Sururu.
                                                       Mwisho





Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Leonard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari jambia na kisu silaha zilizodaiwa kutumika katika tukio la mauaji ya watu 8 kuchinjwa na watu wanaodaiwa kuwa majambazi tarehe 31/05 2016 kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga.


 Kamanda wa Polisi Tanga, Leonard Poul akiwaonyesha waandishi wa habari vyombo mbalimbali na madumu ya kuhifadhia maji yaliyopatikana Mapangoni ambako inasadikika kuwa majambazi walikuwa wakifanya makazi yao .
 Kamanda akiwaonyesha utumbo wa mbuzi waandishi wa habari uliokutwa katika sufuria

 Masanduku ambayo majambazi walikuwa wakihifadhia nguo pia yalikutikana mapangoni
Kamanda wa Polisi Tanga akizungumza na waandishi wa habari kukamatwa kwa vifaa mbalimba vikiwemo majambia visu, mitarimbo ya kuchimbia majabali, sururu na nondo vilivyokutwa ndani ya mapango ya Mleni Amboni Tanga usiku wa jana.

No comments:

Post a Comment