Muuaji wa Jo Cox ajigamba mahakamani
Thomas Mair, mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mbunge wa Uingereza amefikishwa mahakamani Central London.Alipoambiwa aseme jina lake, mtu huyo mwenye umri wa miaka hamsini na mbili alisema nikimnukuu ''jina langu ni kifo kwa wasaliti,uhuru kwa Uingereza''.
Mair pia ameshtakiwa kwa kumdhuru vibaya Cox,kupatikana na bunduki na silaha nyingine hatari.
Marehemu Cox aliyekuwa akiwakilisha chama cha upinzani cha leba alipigwa risasi na kudungwa kisu katika eneo lake la uakilishi siku ya alhamisi.
Kifo chake kimesababisha kusitishwa kwa majuma kadhaa kampeini za kura ya maoini juu ya Uingereza kujiondoa katika uanachama wa muungano wa EU
No comments:
Post a Comment