Korea Kaskazini yadai uwezo wa kulipua Marekani
Kiongozi wa Korea
Kaskazini, Kim Jong Un, amesema kuwa taifa lake linauwezo wa kushambulia
maeneo yote ya Marekani, katika bahari ya Pacific.
Rais Kim Jong
alisema hayo baada ya taifa lake kufanikiwa kutekeleza majaribio ya
makombora yenye uwezo wa kusafiri mwendo wa kasi..Wataalamu wa kijeshi wa Marekani na Korea Kusini wanasema kwamba kombora moja lilishindwa kulipuka ilihali la pili ilifaulu kwenda zaidi ya mamia ya kilomita.
Korea Kaskazini imesifia pakubwa uwezo wake huo wa kuunda silaha za kitonoradi.
Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamekutana na kuelezea kushtushwa kwao na hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
BBC
No comments:
Post a Comment