Thursday, June 23, 2016

WATU 50 WAUWAWA KWA KIMBUNGA CHINA

Zaidi ya watu 50 wauawa na kimbunga China

Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa zaidi ya watu 50 wameauwa kufuatia kutokea kimbunga na mvua kubwa katika mkoa ulio mashariki mwa nchi wa Jiangsu.
Katika maeneo ya mji wa Yanchen kimbunga hicho kilisababisha nyumba kuporomoka na kung'oa laini za umeme.
Sehemu nyingi za nchi zimekumbwa na mvua kubwa wiki hii. Mafuriko kati kati mwa China yamesababisha karibu watu 200,000 kuhama makwao.
BBC

No comments:

Post a Comment