Wednesday, June 22, 2016

BINGWA WA MARATHONI AWA AFISA POLISI KENYA

David Rudisha ni 'afande' Kenya

 
Bingwa wa zamani wa  dunia  mbio za mita 800, David Rudisha ni afisa mkuu wa polisi nchini Kenya? maelfu ya mashabiki wake walipigwa na butwaa alipochapisha picha yake akiwa amevalia sare rasmi ya kikosi cha utumishi kwa wote katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.
Picha hiyo inayomuonesha akiwa amevalia sare ya kikosi cha polisi inadhihirisha kuwa ni afisa wa ngazi ya juu.
Sio aghalabu kuwa bingwa huyo na mshika rekodi wa dunia wa mita 800 kwa upande wa wanaume ni afisa polisi, asilimia kubwa ya wanariadha wakenya ni maafisa wa idara mbali mbali za vikosi vya ulinzi.
BBC

No comments:

Post a Comment