Thursday, June 30, 2016

PROFESA WA IVORY COAST APATA SIFA BAADA YA KUBEBA MTOTO MGONGONI

Profesa aliyebeba mtoto mgongoni apata sifa

h
Profesa mmoja wa chuo kikuu amesifiwa pakubwa nchini Ivory Coast kwa kumbeba mtoto wa mmoja wa wanafunzi wake mgongoni wakati wa masomo.
Picha za Honore Kahi wa chuo cha Bouake, zimesambaa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Alisema aliamua kumsaidia mwanamke katika darasa lake wakati mtoto alianza kulia.
Picha zilizochukuliwa na mwanafunzi mwingine zinamuonyesha, bwana Kahi akifunza huku mtoto akiwa mgongoni.
BBC

No comments:

Post a Comment