Aamka na nyoka kitandani Australia
Nyoka mkubwa ambaye
alikuwa akiishi katika dari ya nyumba moja nchini Australia kwa
takriban miaka 10 sasa ameamua kuingia katika chumba cha kulala.
Mwenye
nyumba hiyo Trina Hibberd kutoka eneo la Queenland aliamka siku ya
jumatatu na kumuona nyoka huyo mwenye urefu wa mita 5.2 amejipinda
katika kitanda chake.Aliwasha taa ya chumba hicho kabla ya mtaalam wa kushika nyoka Dave Goodwin kuwasli.
Goodwin aliidunga sindano ya kulala nyoka hiyo yenye kilo 40 kabla ya kuiweka katika mkono wake na kuondoka nayo.
BBC
No comments:
Post a Comment