Aliyeibuka wa kwanza katika mtihani India afungwa jela
Mwanafunzi wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili.
Ruby
Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo
katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo
la sayansi ya siasa linahusu mapishi.Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.
Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.
Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto.
Gazeti la Hindu lilimnukuu afisa mkuu wa polisi Manu Maharaj akisema kuwa bi Rai atalazimika kubaini kwamba yeye ni mtoto.
Wakati huohuo agizo la kukamtwa limetolewa kwa wanafunzi wengine ambao walifanya vyema katika mtihani akiwemo Sauragh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi lakini ambaye baadaye alishindwa kusema kwamba H20 ni maji.
BBC
No comments:
Post a Comment