Morgan Tsvangirai alazwa hospitalini Afrika Kusini
Kiongozi wa chama
cha MDC chenye upinzani mkubwa nchini Zimbabwe, ambaye aliwai kuwa
waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai, amelazwa katika hospitali
moja nchini Afrika Kusini akipewa matibabu ya saratani ya utumbo .
Chama
cha MDC kimekua kikibana habari hizi kikisema kiongozi wao Morgan
Changarai anasumbuliwa na machofu lakini jana Bw Changirai mwenye umri
wa miaka 64 alitamka rasmi kuwa amekutikana na maradhi ya saratani ya
utumbo (Colon Cancer) na kwamba ameamua kutoa habari hiyo kuhusu afya
yake kwa sababu ni mtu maarufu katika jamii.Kwa sasa Bwana Tsvangirai wiki hii imeanza rasmi kupewa matibabu ya mionzi ya saratani aina ya Chemotherapy katika Hospitali moja nchini Afrika Kusini ambayo haikutajwa jina lake .
Tetesi za kuumwa kwa Bwana Tsvangirai zilianza kuzagaa pale aliposhindwa kuhudhuria mkutano wa chama kuwahutubia wafuasi wa chama chake cha MDC, na baadaye ikaripotiwa kuwa amekuwa akiwahutubia wafuasi wake kupitia simu ya mkononi ilioyoambatanishwa kwenye kipaza sauti.
BBC
No comments:
Post a Comment