Ajali ya EgyptAir kisanduku kuchunguzwa
Wataalam wa
masuala ya anga wamefanikiwa kurekebisha kifaa kinachotunza kumbukumbu
ya mwenendo wa ndege cha EgyptAir iliyoanguka mwezi uliopita na kuua
watu 66 waliokuwamo ndani yake.
Hatua hiyo inawapa nafasi
wachunguzi hao kuweza kuzitafakari na kuzifuatialia taarifa
zitakazobainisha ni kwanini ndege hiyo ilianguka mashariki mwa bahari ya
Mediterranian. Taarifa rasmi kuhusiana na uchunguzi huo zinasema kuwa
kazi ya kusikiliza na kuzifuatilia sauti hizo itafanyika ndani ya saa
chache zijazo. Kisanduku hicho cha mawasiliano kimefikishwa mjini Paris
Ufaransa jana jumatatu kutoka Cairo Misri ambapo kimepelekwa huko ili
kuondoa tabaka za chumvi zilizokizunguka chombo hicho. Hata hivyo
kinatarajiwa kurejeshwa katika maabara za mjini Cairo kwa uchunguzi
zaidi baada ya marekebisho yote kukamilika. Mapema wanasheria nchini
Ufaransa walifungua kesi ya mauaji dhidi ya ajali hiyo kwa madai kuwa
ilitokana na hujuma. Wanasema hakuna uthibitisho wowote kuwa ajali hiyo
ilitokana na ugaidi.BBC
No comments:
Post a Comment