Thursday, June 23, 2016

VARDY AGOMA KUJIUNGA NA ARSENAL

Kama ulitarajia kumuona Vardy akijiunga Arsenal, katoa maamuzi

Najua huenda wewe ulikuwa ni mmoja kati ya watu au mashabiki wa soka waliokuwa wanatarajia kuona mshambuliaji wa timu ya taifa ya England na klabu ya Leicester City Jamie Vardy akijiunga na Arsenal, leo June 23 2016 zimetoka taarifa tofauti.
Taarifa mpya zilizotoka kuhusu stori za Jamie Vardy kujiunga na Arsenal ni kuwa, mshambuliaji huyo ameamua kuendelea na maisha yake ndani ya klabu yake ya sasa ya Leicester City ambao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2015/2016.
Stoke-vs-Leicester
Vardy kwa sasa ameripotiwa leo June 23 kufuta mpango wa kujiunga na klabu ya Arsenal ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kumsajili na badala yake, anatarajiwa kuongeza mkataba wa miaka minne kuendelea kuitumikia Leicester City

No comments:

Post a Comment