Mapacha wenyewe ndio hawa ambapo wote ni wa kike.
Kwa kawaida mapacha wanazaliwa siku moja wakiwa wametofautiana muda
mfupi sana na mara nyingi huwa inakuwa ni sekunde au dakika toka wakati
anapozaliwa mmoja mpaka wakati anakozaliwa mwingine na hii ni kwa sababu
kibaiolojia haiwezekani kwa watoto wawili kutoka tumboni kwa wakati
mmoja.
Lakini Uingereza imeweka rekodi hii ya kuwa na watoto mapacha ambao
siku zao za kuzaliwa ziko kwenye tarehe mbili tofauti yaani kama mmoja
amezaliwa tarehe 1 mwingine amezaliwa tarehe 2.
Huko Bolton watoto Scarlett na Robbyn wameweka rekodi hii baada ya
mama yao kujifungua watoto wawili kwenye tarehe mbili tofauti, ilianza
kama utani wakati ambapo mama huyo aliingia kwenye maumivu ya uchungu wa
kuzaa saa chache kabla ya kuingia kwa siku mpya ambayo kwa mahesabu ya
kidunia huanza saa sita usiku.
Hawa
ni mapacha ambao mwaka 2013 walivunja rekodi ya kuzaliwa katika nchi
mbili tofauti, mmoja alizaliwa England na mwingine Scotland ambapo wa
pili alizaliwa dakika 100 baada ya wa kwanza kuzaliwa.
Kabla ya kufika kwa saa sita kamili usiku majira kama ya 5 na dakika
45 usiku mama huyo alijifungua mtoto mmoja huku akingojea kujifungua
mwingine kwani alifahamu fika amebeba mapacha.
Mtoto mwingine alikuja kuzaliwa dakika 18 baada ya saa sita usiku
kupita na hivyo kufanya ionekane kuwa watoto mapacha Robyn na Scarlett
wamezaliwa kwenye tarehe za siku mbili tofauti mmoja akiwa amezaliwa saa
tano usiku kabla ya siku mpya kuanza na mwingine akiwa amezaliwa baada
ya saa sita usiku saa chache baada ya siku mpya kuanza.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote na Kumekucha blog