Saturday, November 22, 2014

Mgalu afungua Shimmuta, Tanga



Saturday, November 22, 2014

DC MGALU AZINDUA MASHINDANO YA SHIMUTA LEO MKWAKWANI.

MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKIZUNGUMZA LEO WAKATI AKIFUNGUA MASHINDANO YA SHIMUTA MKOANI TANGA


KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKIZUNGUMZA NA WANAMICHEZO KULIA KWAKE NI KATIBU WA SHIMUTA AWARD SAFARI LEO,MASHINDANO HAYO YANASHIRIKISHA WANAMICHEZO 500.

KATIBU WA SHIMUTA,AWARD SAFARI AKIZUNGUMZA NA WANAMICHEZO WANAOSHIRIKI MASHINDANO HAYO LEO WAKATI WA UZINDUZI WAKE
MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKISALIMIANA NA TIMU YA KIWANDA CHA CEMENT CHA TANGA CEMENT LEO

HAPA MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKISALIMIANA NA TIMU YA SOKA CHUO CHA IFM
 





MASHINDANO ya Shimuta yamezinduliwa leo ramsi na Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu ambapo alizitaka mashirika yanayoshiriki mashindan o hayo kuhakikisha wanazingatia taratibu za michuano hiyo kwa kuchezesha wachezaji ambao watakuwa wafanyakazi na sio vyenginevyo.

Mashindano hayo yanashirikisha timu 20 ambazo ni Shirika la Utangazaji  Tanzania (TBC),Chuo Kikuu Huria(OUT),Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE),Kampasi za Mbeya na Dar es Salaam na Mwanza,Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Chuo Kikuu cha Ardhi.

Timu nyengine ambazo zinashiriki mashindano hayo ni Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA),Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini(IRDP),Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA),Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MOCU),Chuo kkikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS),Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Wengine ambao watashiriki kwenye mashindano hayo ni Baraza la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira (NEMC),Shirika la Mzinga,Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC), Wenyeji wa Mashindano hayo,TANGA CEMENT na Timu mpya kwenye shirikisho hilo ya Bohari ya Madawa(Medical Stores Department(MSD).

Kauli mbiu ya Mashindano hayo msimu huu ni "Michezo kuboresha Afya za Wafanyakazi "Tufanye Michezo sehemu za Kazi.

No comments:

Post a Comment