Tuesday, November 25, 2014

Sharo miaka 2 tangu kifo chake


 Miaka miwili tangu Sharo Milionea afariki kwa ajali ya gari

Miaka miwili tangu Sharo Milionea afariki kwa ajali ya gari


.
.
November 26 2014 ni siku ya kumbukumbu ya Sharo Milionea ambae ametimiza miaka miwili toka afariki dunia kwenye ajali ya gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478  BVR alilokua akiliendesha mwenyewe kutoka Dar es salaam kwenda kwao kijijini Lusanga wilaya ya Muhenza Tanga.
.
.
Kama umemis taarifa kuhusu kumbukumbu yake unaweza kutazama post iliyopita


Wakati huu ambapo msanii na mwigizaji marehemu Sharo Milionea anatimiza miaka miwili toka afariki, mmoja wa marafiki zake ambae ni mchekeshaji/Mwigizaji Kitale kupitia instagram alipost picha ya Sharo na kuandika
 ‘ndugu rafiki kipenzi cha watu. #HUSSEIN_RAMADHANI_MKIETI ( sharo milionea ) mwezi kama Huu na tarehe km Hii ndio alitutoka hapa DUNIANI kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la maguzoni mkioni 
TANGA akiwa anaelekea nyumbani kwao kijijini Lusanga wilaya ya MUHEZA. alizaliwa tarehe 28/03/1987 alifariki tarehe 26/11/2012. tokea kifo chake mpaka tarehe kama ya leo ni miaka miwili sasa, ebu 
tuwaombee ndugu zetu na pia tukumbuke na sisi kujiombea ili mwenyezimungu atuepushe na ya DUNIA hapohapo ulipo fumba macho kiimani kabisa kutoka moyoni ukiamini ipo siku mm au ww pia tutakufa omba waombee waliotutangulia mbele za haki ambao leo hii nao walitamani kuwepo istagram lakini awapo na wala awatakuwepo kama mimi na ww tutavyokuja kukosa kuwepo leo au kesho…….wote tuseme ameen.
.
.

No comments:

Post a Comment