Kumekucha Blog
Korogwe,WAKUNGA Wilayani Korogwe Mkoani
Tanga, wameitaka jamii ya mama wajawazito kuwa na ada ya kuhudhuria vituo vya
afya vipindi vya ujauzito na kukemea tabia ya baadhi ya watu kujifungulia
sehemu zisizo tambulika.
Wakizungumza katika mafunzo kwa wakunga vituo vya afya
Wilayani humo juzi,yaliyoandaliwa na Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA) walisema wamekuwa wakipata wakati mgumu
kumpokea mjazito ambaye hajawahi kuhudhuti kliniki.
Walisema kuna baadhi ya wajawazito wamekuwa wakisahau wajibu
wao wa kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito na hivyo kipindi cha kujifungua hufika
vituo vya afya na kuwa shida baada ya kutokuwa na kumbukumbu za ujauzito huo.
“Tuko na changamoto nyingi sisi wakunga hasa pale ambapo mama
mjamzito anapofika siku ya kupata uchungu wa uzazi na hivyo kushindwa namna ya
kumpokea” Chevu Mkufya
Alisema ili kujiepusha na matatizo wakati wa kujifungua
amewataka mama wajawazito kuhakikisha wanapopata ujauzito tu kuanza kliniki na
kudai kuwa hiyo itasaidia kupunguza vifo vya mtoto wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mratibu wa wafunzo hayo Martha Rimoi aliwataka
watumishi hao kuwa mabalozi wazuri katika vituo vyao lengo likiwa ni kutokomeza
vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Alisema kufuatia kukithiri wimbi la wasichana kuzaa muda umri
mdogo ni wajibu wa wakunga kutoa elimu mashuleni na kwa njia ya televisheni
katika maeneo ya wazi ili kila mmoja kutambua wajibu wake.
“Ninyi wakunga ndio muonaojua kero ambazo munakabiliana nazo
hebu jipangeni na hata kuomba bajeti ili kuandaa vipindi vya maonyesho vya
televisheni jamii itambue ubaya na uzuri mjazito nini anatakiwa kufanya”
alisema
“Mimba za utotoni zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku hivyo
ni vyema kuwa na utaratibu wa kutoa elimu mashuleni na katika viwanja vya wa
wazi na kusaidia kutokomeza matatizo ya wazazi wakati wa kujifungua” alisema
Rimoi
Alisema kufanya hivyo kutasaidia kuwafanya wazazi na
wajawazito kutambua wajibu wao vipindi vya kubebea ujauzito na hivyo kuwataka
kuwa na mikakati ya kulimaliza tatizo hilo kwa wajawazito.
Mwisho
No comments:
Post a Comment