Usafiri wa mkokoteni umekuwa mkombozi kwa watu wa kipito cha chini na hivyo kuutumia kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kusafirisha bidhaa na thamani za ndani kama ambavyo wanaonekana vijana hawa wa mtaa wa chumvini kata ya Chumbageni Tanga leo asubuhi.
Ndio kama hivyo wamo katika kuwajibika na kupeleka vitu hivyo vya thamani ambvyo kuna jamaa amehama sehemu aliyokuwa ila haieleweki kama amehama kwa ridhaa yake au amehamishwa kwa nguvu si unajua kuwa nyumba kama sio yako huna raha nayo
Mfanyabiashara wa bodaboda Tanga akimpita dereva wa mkokoteni eneo la Chumvini kata ya Chumbageni Tanga leo asubuhi.
Vijana hawa wamo katika uwajibikaji wa kupeleka vyombo ila haijulikanani wanapeleka wapi inawezekana anahamia mjengoni kwake au amepigwa patresheni alikokuweko awali.
Mchuuzi wa samaki akiwa na baskeli yake ikiwa amesheheni dagaa aina ya Uwono huku mbele yake akipishana na madreva wa mkokoteni ulojaa thamani za ndani eneo la Chumvini kata ya Chumbageni Tanga mapema asubuhi hii. Mmiliki wa Blog hii ni Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Tanga, 0655 902929
No comments:
Post a Comment