Arsenal wachoshwa na Wenger
Mashabiki wa Arsenal wamezungumza na kama sauti yao itasikika basi huenda siku za Arsene Wenger kama kocha wa klabu hiyo ya London zinahesibika .
Hii ni baada ya mashabiki wa timu hiyo kuonyesha kuwa wamechoshwa na hali ya timu hiyo kuwa nyuma ya timu nyingine .
Mabango yaliyoonekana kwenye uwanja wa Hawthorns hapo jana wakati Arsenal ikiwa inacheza na West Bromwich Albion yalionyesha ujumbe ulioandikwa hivi ‘Arsene Wenger We Thank You For The Memories , But Its Time To Say Goodbye, ‘Yaani Asante kwa kumbukumbu nzuri lakini muda wa kuagana na wewe sasa umewadia’.
Kauli hii ya mashabiki wa Arsenal inakuja baada ya timu hiyo kujikuta ikiwa nyuma ya vinara wa ligi kuu ya England Chelsea huku kukiwa na pointi 13 na nafasi tano ambazo zimezitofautisha timu hizi mbili .
Zaidi ya hapo mashabiki hao wakiingalia timu yao hawaoni kama wana matumaini ya kweli ya kutwaa ubingwa wa ulaya au kufika mbali kama vile nusu fainali , au fainali .
Tangu Arsenal walipotwaa taji la ligi kwa mara ya mwisho imepita miaka kumi na pamoja na kutwaa ubingwa wa kombe la Fa msimu uliopita bado mashabiki hawaoni kama chini ya Mfaransa huyu kuna matumaini ya kweli ya kufikia kilele cha mafanikio kama ilivyo kwa timu za Manchester City , Chelsea na Manchester United .
No comments:
Post a Comment