Novemba 26 Bungeni Tz, ishu ya Escrow na agizo la Mahakama kuzuia mjadala wa Ripoti ya CAG
Wakati Kikao cha Bunge kikiendelea
Dodoma leo, miongozo bado iliendelea kuombwa na baadhi ya Wabunge
kuhusiana na suala ambalo limechukua siku kadhaa sasa kwamba Mahakama
ilitoa agizo la kuzuia Bunge kujadili kuhusiana na Ripoti ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu Wa Serikali CAG, leo Novemba 26 Wabunge Suleiman Nchambi,
Esther Bulaya, Tundu Lissu, Ole Sendeka na Joshua Nassari waliomba
mwongozo kuhusiana na hilo.
Mbunge Nchambi alianza kwa kuuliza; “…
Watanzania waelewe wazi sisi wabunge wa Chama cha Mapinduzi tunayo
dhamira ya kujadili jambo hili Bungeni na kwa kuwa CHADEMA wameonyesha
waziwazi kupitia mjumbe wao kuwa wanapinga suala hili, naomba mwongozo
wako kwanini wakati tunajadili suala hili zito tusijadili pia suala hili
zito la mjumbe wa CHADEMA kwenda kupinga kujadiliwa hoja hiyo hapa
Bungeni…”
Tundu Lissu akajibu hoja hiyo; “… Anaitwa Gabriel Mnyele,
mkazi wa Mpanda ni mwana-CCM na wasiofahamu mimi nimesoma naye… Wakili
wa Pan African Power Solutioms anafanya kazi kwenye kampuni moja ya
uwakili na Mabere Marando, isipokuwa Wakili Mabere Marando hajahusika kwa namna yoyote ile na kesi iliyopelekwa Mahakamani...”
Kuusikiliza mjadala huo wa Bunge bonyeza play hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati
wowote.
No comments:
Post a Comment