Thursday, November 27, 2014

Lori labamiza Costa na kuua 11, Muheza

Kumekucha Blog

WATU 11 wamekufa papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi  dogo
kugongana uso kwa uso na lori aina ya  Scania katika kijiji cha Mkanyageni,
wilayani Muheza, Mkoani Tanga.


Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1 asubuhi ilihusu basi aina ya
Coaster lililokuwa linakwenda Lushoto kugongana na lori hilo la Scania
ambalo lilikuwa linakwenda Tanga mjini.


Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dr. Peter Mwankai miili ya
marehemu hao 11 imehifadhiwa katika Hospitali Teule Muheza na tayari miili
ya abiria saba waliokufa imekwisha tambuliwa.


Waliotambuliwa ni Moodi Muhamed , Zawadi Juma, Sister Christina, Ahmed
Shemdoe, Asumani Masanja, Adam Shomari and Saumu Hassan. Miili ya abiaria
wengine watatu bado haijatambuliwa.


Majeruhi 22  ambao baadhi yao wameumia katika sehemu za mikono na miguu
wamekwisha tambuliwa.


Majina ya majeruhi yalitajwa kuwa Ambrose Benedicto, Heri  Frenimo,
Ramadhani Kawote, Mmwananisha Hamdani, Hidaya Mohamed, Hassan Juma, Allan
Charles, Paulo Moshi, Saleh Ali, Clara Lupari, Mwanaisha Rajabu, Abubakari
Salimu, Richard Kitala, Mwajuma Kasongo, Bahati Hussein, Mtaita Shangwe,
Benjamin Abedi (Dereva), Ramadhani Othman, John Fumeena, Ali Ibrahim.


Kwa mujibu wa dereva wa basi dogo la Coaster, *Bakari* Mussa, chanzo cha
ajali ni dereva wa lori kuwa katika mwendokasi na kushindwa kudhibiti gari
ambalo lilianza kwenda upande wake.


Alidai alijitahidi kulikwepamlori hilo lakini lilizidi kuja uoande wake na
hivyo kugongana uso kwa uso. Dereva wa  lori aliyetambuliwa kwa jina la
Benjamin Abedi pia ni miongoni mwa majeruhi.

                                        Mwish

No comments:

Post a Comment