Manchester City yawaadhibu ‘Watakatifu’.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City wamehsinda mchezo wao wa ligi kuu ya England baada ya kuwafunga Southampton au The Saints Aka Watakatifu kwa matokeo ya 3-0 .
Manchester ambayo ililazimika kumaliza mchezo huo ikiwa na watu nane uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa beki wake Mfaransa Eliaquim Mangala na kuumia kwa nahodha wake Vincent Kompany walipata bao la kwanza mapema kwenye kipindi cha pili mfungaji akiwa Yaya Toure .
City walifunga bao la pili kupitia kwa mkongwe Frank Lampard kabla beki Gael Clichy hajamalizia bao la tatu .
Ushindi huo unawafanya City kusogea hadi nafasi ya pili toka nafasi ya tatu walikokuwa ambapo wamewaondoa Southampton kwenye nafasi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 27 baada ya michezo 13.
No comments:
Post a Comment