Thursday, November 27, 2014

Etto, aachana na Ukapera

Unamjua staa wa Soka Duniani ambaye amefunga ndoa hivi karibuni?

Wedding-Hands1Samuel Eto’o, moja kati ya wachezaji wakubwa wa  soka duniani  amefunga ndoa rasmi baada ya kuishi na mwanamke huyo ambaye walifunga ndoa ya kimila tangu mwaka 2007.
Eto’o amefunga ndoa na Tra Lou Georgette ambaye ana asili ya Ivory Coast na tayari wana watoto wanne.
Huenda kutokana na ustaa wake ungetarajia kuona tukio kubwa sana katika siku ya sherehe yao, lakini taarifa zinasema walifunga ndoa na kufanya sherehe ya kawaida sana katika mji wa Como, Italy siku ya jumatatu November 24.
Huenda katika sherehe hii cha thamani kubwa ikawa ni pete ya almasi ambayo Eto’o alimvisha mpenzi wake huyo Mwezi July, ambayo thamani yake ni Euro 500,000.
Samuel-Etoo-Georgette-600x600
samuel-etoo-wedding

No comments:

Post a Comment