Katika kikao cha Bunge leo Novemba 21,
Mbunge Peter Msigwa aliuliza swali kuhusiana na kitendo cha Mawaziri na
Wabunge kutosomesha watoto wao wala kutotibiwa ndani ya Nchi; “…Tafiti
zinaonesha kwamba wale watu ambao ni wataalamu hawarudi kwenye maeneo
yao.. Kwa kuwa katika sekta ya elimu na afya imeonyesha kwamba viongozi
kuanzia Mawaziri pamoja na Wabunge hawaamini mfumo wa elimu ndio maana
hawapeleki watoto wao kwenye shule hizo za Serikali ..
“..Hata
Mawaziri wenyewe hawaamioni mfumo wa afya ndio maana na wenyewe
hawatibiwi kwenye Hospitali za nchini, pamoja na Wabunge. Je haoni ni
wakati muafaka sasa kwa Serikali kuleta sheria ambayo italazimisha
Waziri, Wabunge wanaohusiana na Sekta hizi walazimishwe kusomesha watoto
wao na kutibiwa katika Hospitali hizo wanazoziongoza ili kuleta adabu
na ufanisi katika utendaji kusudi wananchi watuamini kwamba Tunaongoza
Sekta ambazo na sisi wenyewe tunaziamini…“– Msigwa.
Akijibu swali hilo Waziri Celina Kombani amesema; “…
Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Msigwa ambalo limetoka nje ya Mada
kama ifuatavyo; kiongozi ni mfano kwa hiyo Mheshimiwa Msigwa anaweza
akaanza yeye kutibiwa kwenye Hospitali za kawaida, akawa ni mfano kwa
wengine, basi na wengine tutafuata…“
No comments:
Post a Comment