Sunday, November 23, 2014
Pata muktasari wa dondoo za magazeti ya leo
NIPASHE
Katika hali isiyokua ya kawaida Zahanati ya Matanga Manispaa ya Sumbawanga ina muuguzi mmoja tu ambaye anafanya kazi za kupima wagonjwa,kutoa dawa na kuzalisha kina mama kwa kutumia mwanga wa kibatari
.
Muuguzi huyo Bruno Ntalyoka mwenye miaka 40 amefanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya daktari wa Zahanati hiyo kuhamishwa na yeye kushikilia nafasi hiyo hadi leo.
Ntalyoka alisema alianza kazi mwaka1985 na hospitali hiyo ilikua na daktari mmoja na yeye alikua akimsaidia lakini baada ya kuhamishwa yeye alikua akifanya kazi zake zote.
“Nafanya kazi vizuri tu na hakuna tatizo lolote wala malalamiko kutoka kwa wananchi,naamini haya yote yatakwisha baada ya Serikali kuleta daktari mwingine.
Alisema inapotokea mama mjamzito anataka kujifungua husitisha shughuli zote kwa wakati huo na kuanza kumuhudumia na kwa kawaida kila mwezi huzalisha wajawazito18 ambao ni swa na wastani wa wanawake wawili mpaka watatu kwa siku.
Alisema kazi hiyo inakua ngumu usiku kwa sababu Zahanati hiyo haina umeme kwa muda mrefu sasa hivyo humbidi kutumia mwanga wa kibatari kuwahudumia wakina mama hao
MWANANCHI
Waziri wa zamani katika Serikali ya awamu ya pili na ya tatu,Mateo Quaresi amesema kwamba Chama cha Mapinduzi CCM kwa sasa hakina mgombea mwenye sifa wa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania.
Mwanasiasa huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Babati kwa tiketi ya CCM,alisema kuwa Chama hicho hakiwezi kutoa rais bora anayeweza kuwavusha Watanzania walipo sasa nakuwapeleka mahali pazuri zaidi kwa sababu ina viongozi wasiojiamini,hawawezi kutoa uamuzi mgumu katika kuiongoza nchi.
“Mpaka sasa watu wanaotajwa tajwa kuwania urais kwa upande wa CCM mimi naona hakuna mwenye sifa kwa sababu CCM haiwezi kumpitisha kiongozi mzuri na mwadilifu kwa kuwa watu wanatumia fedha na hawezi kupata kiongozi mzuri kwa kutumia fedha”alisema Quaresi.
Hata hivyo alisema kazi ya urais ni ngumu na si ya mchezo kama wanavyodhani baadhi ya watu na ndio maana unaona mtu hajamaliza hata miaka mitano anatangaza nia ya kutaka kugombea urais.
MWANANCHI
Ripoti ya sakata la ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow sasa itajadiliwa kwa siku mbili bungeni baada ya kikao cha kamati ya uongozi ya bunge kukubaliana kuongeza muda tofauti na ule wa awali ambao ulikua hautoshi.
Ripoti hiyo ambayo ilipitiwa na kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali ‘PAC’,awali ilitakiwa kusalishwa bungeni tarehe27 wiki ijayo na kujadiliwa siku hiyo hiyo.
Baadhi ya Wenyeviti wa kamati mbalimbali za bunge ambao ni wajumbe wa kamati ya uongozi walisema kuwa wamejadiliana na kukubaliana kuwa muda uongezwe kwani siku moja haitoshi.
Suala la muda mdogo wa kuwasilisha na kujadiliwa kwa ripoti hiyo bungeni umelalamikiwa na baadhi ya wabunge ambapo Mbunge James Mbatia na Livingstone Lusinde walikitaka kiti cha spika kutoa muda wa wiki nzima kujadili sakata hilo ili wamalizane nalo.
MWANANCHI
Mgogoro wa ardhi Wilayani Kiteto jana umechukua sura mpya baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Martha Umbulla kumshambulia mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM NEC Emanuel Papian kuwa ni mmoja wa wachochezi wa mapigano ya ardhi.
Umbulla alitoa kauli hiyo katika mkutano wa kusaka muafaka ambao uliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Erasto Mbwillo na kushirikisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani Manyara na viongozi wote wa kata zenye migogoro.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema mjumbe huyo ambaye ni mmoja wa wakulima wakubwa Wilayani humo amefikia hatua ya kuwalipa fedha vijana kwa ajili ya kuandaa mabango ya kumpinga yeye na Mbunge wa jimbo hilo Benedict Nang’oro.
Alisema siri ya mpango huo uligunduliwa na katibu wa Uenezi Nape Nnauye baada ya kuwahoji vijana waliokua wamebeba mabango hayo.
MZALENDO
Polisi wamemshikilia kijana aliyekua akifanya mapenzi na sanamu ya kuchezea watoto ndani ya Supermarket moja nchini Marekani.
Sean Johnson mwenye miaka19 alikamatwa na jeshi hilo baada ya kunaswa na wanunuzi wa bidhaa ndani ya Supermarket hiyo ya Walmart akiwa uchi huku akifanya ngono na mwanamke mwenye maumbile ya kike.
Taarifa ya jeshi hilo ilisema Johnson alikamatwa katika video iliyomuonyesha akiwa yupo busy na sanamu hiyo hadi alipogundulika na baadhi ya watu waliokua wakinua bidhaa.
Inasemekana alipokamatwa aliomba radhi lakini wateja walikataa na kumkokota hadi polisi pamoja na sanamu alilokua akifanya nalo kitendo hicho.
MZALENDO
Genge hatari limeibuka Dar ambapo limeua kinyama wasichana wawili marafiki na miili yao kutupwa maeneo tofauti.
Wasichana waliouawa ni Wanze Makongoro mwenye miak na23 ambaye ni mpwa wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mecky Sadicky na Jackline Masanja ‘Salha’ aliyewahi kusikika katika ipindi chanjiapanda kinachorushwa na kituo cha ClaudsFm.
Usiku wa kuamkia November13 inadaiwa Wanze aliwaaga marafiki zake kuwa anakwenda kutengeneza simu Mlimani City na hakuweza kurudi tena hadi mwili wake ulipookotwa katika mto Msimbazi na kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya Muhimbili.
Kutokanana tukio hilo jeshi la Polisi Dar limeingia katika lawama kupitia kwa ndugu wa marehemu huyo kwani tangu msichana huyo alipopotea na ndugu kutoa taarifa hawakuweza kupata taarifa yoyote hadi walipofika Muhimbili na kukuta mwili wake.
HABARILEO
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani,Nurdin Babu ameagiza wanafunzi24 wa Sekondari mbalimbali Wilayani humo waliopata ujauzito kuripoti kituo cha polisi November25 mwaka huu ili wasaidie kutoa ushirikiano wa kuwakamata wahusika waliowapa mimba na kuweze kukamatwa.
Sambamba na wanafunzi hao pia wazazi au walezi wa wanafunzi hao wametakiwa kuripoti wakiwa na watoto wao ambapo atazungumza na wazazi pamoja na wanafunzi hao ili kujua tatizo ni nini.
Babu alisema taarifa za watoto26 walipata ujauzito katika kipindi cha Januari hadi Oktoba si nzuri na lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe ili kuondokana na matatizo hayo ndani ya jamii.
Alisema idadi ya wanafunzi waliokatishiwa masomo ni kubwa na Serikali haiwezi kulifumbia macho suala hilo.
NIPASHE
Wabunge wa Chama chaMapinduzi CCM wamemtaka Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kujiuzulu ili kuisafisha Serikali dhidi ya kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL ya uchotwaji wa shilingi bilioni306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo benki kuu ya Tanzania BoT.
Ushauri wa kumtaka jaji Werema ajiuzulu ulitolewa na baadhi ya wabunge katika kikao cha kamati ya uongozi ya wabunge wa Chama hicho kilichofanyika mjini Dodoma.
Walisema sakata hilo la wizi wa mamilioni limeichafua Serikali na kujiuzulu kwake kutaleta unafuu na kwani uamuzi huo ni dhahiri kuwa fedha zilizokua zimehifadhiwa kwenye akaunti hiyo zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na TANASCO.
Kumekucha Blog itakuhabarisha yanayojiri magazetini kila siku, usikubali uhondo huuu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment