Tuesday, November 18, 2014

Wachimba kisima baada ya kuchoshwa na ahadi hewa ya Serikali

Kumekucha, Blog

Pangani,WAKAZI wa kijiji cha Mkalamo Wilayani Pangani Mkoani Tanga, wamesema wamechoshwa na ahadi ya Serikali kuwachimbia kisima cha maji safi kijijini hapo na hivyo kuadhimia kuchangishana na kuchimba kwa gharama zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa blog hii, wakazi hao walisema kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikitoa ahadi  hewa za kuchimba kisima lakini hadi muda huo hakuna dalili zozote za utekelezaji.

Walisema kufuatia kusuasua huko na wakazi wengi  eneo hilo kuteseka kwa kuyafuata maji umbali mrefu na kuamua kuchangishana kwa kila nyumba kuchangia elfu 20 na kufikisha lengo ambalo wamejiwekea.

“Kipindi kirefu tumekuwa tukiahidiwa kuchimbiwa kisima na hata viongozi wa ngazi za juu nao ni wamoja wapo----hadi sasa hakuna dalili ya ahadi hiyo na kuamua ni vyema tukachangishana wenyewe kwa wenyewe” alisema Rashid Sinani

“Kero tunaijua sisi wenyewe na sio wakuja na ndio maana tunataka kuchangishana wenyewe kwa wenyewe---tuko na imani kuwa tutachimba kisima kwa nguvu zetu” alisema Sinani

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Perani, Juma Kolombo amewashauri viongozi wa Serikali za vijiji na vitongoji kuzifikisha kero za wananchi katika ngazi husika na kuacha kuzikalia katika makabati.

Alisema kuna baadhi ya viongozi wengi wanashindwa kuwajibika na badala yake wamekuwa mzigo kwa wananchi na hivyo kuwataka kubadilika vyengine mkakati wa kuwondosha kwa vikao vya vijiji utafuatwa.

“Kuna viongozi wamekuwa mzoigo wanashindwa hata kupeleka barua za wananchi ngazi za juu---hiyo nadhani ni woga wa kupoteza kibarua chake lakini hatambui kuwa ndio kuwajibika” alisema Kolombo

Aliwataja viongozi hao kuwa ni mzigo kutokana na kutofikisha kero zao hata ngazi za kijiji na hivyo kuona kuwa kibarua ambacho wamepewa na wananchi kupitia masanduku ya kura kimewashinda.

Alisema kipindi cha kufanya hivyo ni chaguzi za Serikali za mitaa mabzo ziko karibu na hivyo kuwataka kuwajibika na kuonyesha moyo kabla ya kipindi hicho kufika vyengine wananchi wanaweza kufanya maamuzi tofauti na wanavyofikiria.

                                                 Mwisho


No comments:

Post a Comment