Saturday, November 22, 2014

Arsenal yaendelea kuboronga

 Arsenal vs Manchester United

IMG_8974.JPG
Mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu wa ligi kuu ya England kati ya Man United dhidi ya Arsenal umemalizika jana usiku

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Emirates umemalizika kwa matokeo ya kushtusha kwa watu wengi.
Manchester United waliokuwa wakipewa nafasi ndogo ya ushindi wameondoka na ushindi wa kwanza wa ugenini msimu huu.

Magoli ya Wayne Rooney na Goli la kujifunga la Kieran Gibbs yameipa United ushindi.
Oliver Giroud alifunga goli la kufutia machozi Arsenal.

Angel Di Maria alikosa nafasi ya wazi kabisa kufunga goli la 3 alipobaki na kipa wa Arsenal ambapo aliubetua mpira na ukaenda nje ya lango.

Kwa ushindi huo Man United sasa wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

No comments:

Post a Comment