Sunday, November 30, 2014

Babu amtwanga kijana wa miaka 29 uliongoni




Pale ambapo babu wa miaka 62 anampiga kijana wa miaka 29 kwenye ulingo wa ngumi.


Boxing-GlovesUle msemo wa ng’ombe hazeeki maini au ule wa kiingereza ‘Old is Gold’ naweza kusema ni kama una ukweli kwa kulirejea tukio hili ambalo ni la aina yake.
Kijana wa miaka 29, Elliot Seymour ambaye damu inachemka alijikuta katika wakati mgumu kwenye uliongo wa mchezo wa ngumi pale aliposhindwa kujitutumua mbele ya mzee, kikongwe Mickey Rourke ambaye ni bondia wa zamani na pia muigizaji wa Holywood.
Katika pambano hilo ambalo lilifanyika siku ya ijumaa Marekani, kwanza lilikuwa na kiingilio kikubwa, pili lilikuwa na mvuto wa aina yake ambapo watu walihitaji kupata jibu kati ya babu wa miaka 62 na jamaa wa miaka 29 nani atamshinda mwenzake.
2393FAC000000578-2854714-image-12_1417340313447
Babu alimpiga Seymour kwenye round ya pili ya mchezo, amekuwa gumzo kubwa mitandaoni.
Nimekuwekea video hapa uutazame ushindi wa Babu huyo.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, Kumekucha Blog

No comments:

Post a Comment