Kumekucha Blog
Korogwe, SIKU nne tangu itokee ajali mbaya
iliyohusisha basi dogo la abiria na lori
Muheza Mkoani Tanga na kuuwa watu 13 na
wengine 25 kujeruhiwa jana gari la mizigo lilillojaza watu lilipoteza njia na
kuuwa watu 7 na wengine 14 kujeruhiwa.
Ajali hiyo ilitokea saa 1 jioni kijiji cha Magundi kata ya
Mbungu watu waliokuwa wakitokea mnadani waliokuwa
wamejazana katika gari aina ya Mistubishi Canter iliacha njia na kupinduka na
kusababisha vifo vya watu 7 papo hapo.
Ajali hiyo iliyothibitishwa na kamanda wa polisi Mkoa wa
Tanga, Fraisser Kashai na kuwataja watu waliofariki kuwani, Ali Juma (47), Kihiyo
Rutha, Merina Kiteleko, Asha Mussa, Stella Chales(32) Mama
Kivula na Jane Mbajo na miili yote imehifadhiwa hospitali ya Wilaya ya Magunga.
Kamanda Kashai aliwataja waliojeruhiwa Este Akili, Amina
Mohammed (23), Ramadhani Omar (32)Amina Rajab(32) Veronica Daniel (18), Mwaliki
Pitter, Jarnet Chales(40), Mariama Sadick (45), Said Salinza (42) Mgoshi
Bashiri (48) Monica Chales(40), Veronica Kiondo (43), Zaina Hamis(24) na Richard Mosess.
Akieleza chanzo cha ajali hiyo kamanda Kashai alisema Polisi
inamshikilia dereva wa gari hilo, Ramadhani
Omar kwa uvunjifu wa sheria za barabarani baada ya kuchukua abiria kinyume na
sheria.
Alisema dereva huo alipatwa na tamaa ya kupata pesa baada ya
kumaliza kasi yake ya kupeleka mazao masokoni na bidhaa katika minada hivyo
kuchukua abiria kinyume na sheria.
Alisema watu hao ambao walikuwa wengi dereva huyo alishindwa
kulimudu gari lake na wakati akikata kona ilimshinda na kuingia porini kisha
kupinduka na watu saba kufa papo hapo.
“Tulitoa agizo kuwa magari ambayo hayaruhusiwi kubeba abiria
kuacha kufanya hivyo---lakini agizo hili naona halitekelezwi na hivyo sasa ni
kazi moja tu ya kufikishana mahakamani” alisema Kashai
Akitoa agizo kwa wananchi kamanda huyo amewataka kutoa
taarifa kwa jeshi la polisi pale wanapoona sheria za barabarani zikikiukwa
ikiwa na pamoja na mwendo kasi na upakiaji wa abiri kupindukia.
Mwisho
No comments:
Post a Comment