Tuesday, November 25, 2014

Chama Cha Wauguzi Tanzania chawapa somo wauguzi Korogwe

 Wauguzi mbalimbali hispotali na vituo vya Afya Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kongamano hilo kufungulia na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, Mrisho Gambo alievaa Suti katikati..Na wa mwisho kushoto ni Muuguzi Mkufunzi kutoka Chuo Cha Muhimbili Dar es Salaam
 Kongamano hilo la utoaji wa elimu kwa wauguzi hospitali na Zahanati Wilayani humo liliandaliwa na Chama cha Wauguzi Tanzania (TAMA) kwa ufadhili wa Shirika la Sanof Expour na kumshirikisha Muuguzi Mstaafu kutoka Canada kama anavyooneka hapa katikaipicha akiwa ameshikilia Camera.
 Muuguzi Mkufunzi, Elizabert Mwakalinga akiangalia picha kwenye simu inayoonyesha madhara ya wazazi wanaojifungulia katika vituo ambayo sio vya kutolea huduma na hivyo wazazi kukumbana na changamoto nyingi zikiwemo za kupoteza watoto na mzazi
 Elizabert Mwakalinga anaendelea kuishangaa picha hiyo ambayo ilikuwa ikihuzunisha na kuwashauri wanafunzi wauguzi katika darasa hilo kutoa elimu majumbani ili mzazi mjamzito kuwa na ada ya kuhudhuria vituo vya Afya.
 Mkufunzi Muuguzi, Elizabert Mwakalinga akitoa somo katika darasa la Elimu kwa wauguzi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wauguzi Tanzania (TAMA)
 Wauguzi kutoka vituo mbalimbali Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakifuatilia masomo, Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wauguzi Tanzania (TAMA)
Mratibu wa mafunzo hayo, Martha Rimoi alikuwa bega kwa bega na wakufunzi kuhakikisha kila kitu kinaenda vyema na hata pale alipokuwa na mchango hakuwa nyuma alikuwa akiongezea na kujibu maswali kwa washiriki kama anavyoonekana hapa kushoto alievaa miwani.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwa kushirikiana na mdau kutoka Canada pamoja na Shirika la SANOF

Picha zote na Kumekucha Blog

No comments:

Post a Comment