Mkusanyiko wa Stori kubwa kwenye Magazeti ya leo Novemba 30 ,2014 nimekuwekea hapa
MTANZANIA
Rais Jakaya Kikwete amesema anahitaji kulielewa vyema sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow kabla ya kulizungumzia.
Akizungumza Jijini Dar es salam jana katika uwanja wa ndege JNIA baada ya kurejea kutoka Marekani alikokua akitibiwa matibabu ya kansa alisema ana afya njema na hatoweza kugusia masuala yaliyokua yakiendelea kwa kuwa hajajua cha kusema.
“Ndugu zangu basi ndio hayo,siyasemi ya Dodoma kwa kuwa siyajui vyema nikiyapata nitajua chakusema,”alisema Kikwete.
Kikwete ameshindwa kuzungumzia suala hilo lililosababisha bunge kuahirishwa mara tatu jana kutokana na mvutano wa Wabunge wa namna ya kuyaweka maazimio ya kumwajibisha Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema.
MTANZANIA
Watu wanne wamefariki dunia jana katika ajali ya helkopta iliyoanguka jana katika eneo la Ukonga wakati ikiwa katika ukaguzi wa majaribio.
Helkopta hiyo inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii ilikua ikiendeshwa na marubani wanne kutoka Jeshi la Polisi na Wizara hiyo.
Akizungumza jana Kamishna wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema Helkopta hiyo iliruka kutoka uwanja wa ndege wa JNIA kwa lengo la kuzunguka maeneo ya karibu ili ifanyiwe majaribio.
“Baada ya Helkopta hiyo kuruka uwanja wa ndege kwa ajili yakufanya majaribio,baadaye ikapoteza mwelekeo na kugonga nguzo ya umeme,imeanguka mtaani katika eneo la barabara,”alisema Kova.
Kova alisema ajali hiyo pamoja nakupoteza maisha ya watu ambao maiti zao zimehifadhiwa katika hospitali ya Muhimbili,pia imeharibu vibaya Helkopta hiyo.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete amerejea nchini kutoka kwenye matibabu na kuwaeleza Watanzania kuwa alikua akiumwa saratani ya tezi dume.
Kikwete alisema binafsi hakutaka kufanya ugonjwa huo kuwa siri,lakini alishauriwa kutotangaza ugonjwa huoili asiwatie wananchi hofu na kwa sasahali yake kiafya ni nzuri.
Alisema madaktari walimshauri kufanya upasuaji lakini alilazimika kuomba kufanyiwa Julai2014 ili kupata muda wa kupokea rasimu ya katiba,hata hivyo kwa kuwa bunge la katiba halikuisha kama ilivyotarajiwa aliomba kufanyiwa mwezi huu.
Pia Kikwete alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa madaktari wa hospitali ya Johns Hospkings wamethibitisha ingawa atapaswa kupumzika kwa wiki nne kabla ya kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
MWANANCHI
Chama cha Mapinduzi Wilayani Tabora kimeilaumu Serikali kwa kushindwa kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Katibu wa CCM Tabora Bakari Mfaume alisema Serikali haikuwahamasisha wananchi ipasavyo kujiandikisha ili waone umuhimu wa kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka.
Alisema iwapo Serikali ingewahamasissha ipasavyo dadi kubwa ya wananchi wangejitokeza kujiandikisha tofauti na sasa kwani watu wengi hawasajahamasika.
Hata hivyo amewatahadharisha wananchi ambao watajiandikisha zaidi ya mara moja kuchukuliwa hatua kali za kisheria pindi watakapogundulika.
MWANANCHI
Wasomi ,wanasiasa na wananchi wamepongeza mapendekezo mapya ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC yanayoazimia kuwawajibisha wale wote wanaohusika na kuchotwa kwa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe akisoma mapendekezo manane yaliyokubaliwa na pande tatu ya PAC,kambi ya upinzani na Serikali alisema kila aliyehusika na sakata hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Miongoni mwa watakaohusika na azimio hilo ni Waziri wa Nishati Sospeter Muhongo,Katibu wake Eliakim Maswi,Waziri wa Ardhi Anna Tibaijukana mwanasheria mkuu Fredrick Werema ambao imependekezwa na Mamlaka husika kutengua uteuzi wao.
Baadhi ya wananchi walisema fedha hizo zinatakiwa kurudishwa na zielekezwe kulipa madeni katika bohari kuu ya dawa.kununua vifaa tiba na kuboresha sekta nzima za afya kwa manufaa ya Watanzania walio wengi.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Kumekucha Blog
No comments:
Post a Comment