Matukio ya picha wakati wa uwasilishaji wa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Dodoma
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akiongozana na Mbunge wa
Jimbo la Tabora Mjini,Mhe. Ismail Aden Rage wakati akiwasili bungeni
kuwasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti
ya ESCROW.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati
akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa
kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akienda
kusoma Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa
Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma
leo.
Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya CAG.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia
ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni leo na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya GAG.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe DEO Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge
mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka kesho ambapo Serikali inatarajiwa
kutoa majibu.
Naibu Waziri wa Nishati na
Madini,Mhe. Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya Bunge kuahirishwa. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii
kanda ya kati
sawa
ReplyDelete