Wednesday, November 26, 2014

Ripoti maadhimisho ya usalama barabarani


Ripoti aliyokabidhiwa Mwakyembe kuhusu ajali za Barabarani

police-accident-sign (1)Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe amekabidhiwa Ripoti ya kamati iliyoundwa kutathmini na kutoa mapendekezo hatua ya kuchukua ili kupunguza ajali za barabarani.
Kamati hiyo iliyoundwa na watu 14 imebaini changamoto zinazopelekea ajali hizo kuwa ni pamoja na ratiba za mabasi zinazotolewa na SUMATRA kutozingatiwa pamoja na utaratibu mbovu wa utoaji wa leseni.
Akizungumza wakati wa kupokea Ripoti hiyo Mwakyembe amesema; “… Ajali nchini zinasababishwa na Mwendokasi na uendeshaji hatarishi au kwa maneno mengine uzembe. Waziri Gaudensia Kabaka yeye tayari Wizara yake imefanya kazi kubwa kweli, wamekuja wao na ratiba kabisa ya ukaguzi wa kampuni zote za mabasi na malori, ni ratiba ya miezi miwili kuchunguza mikataba ya kazi kwa upande wa madereva kwa mwezi Desemba na Januari, inasubiri tu Waziri aseme tunaanza tarehe fulani.  
Kwa hiyo siyo tu mikataba ya kazi inaangaliwa, itaangaliwa mpaka na michango ya mwajiri au waajiri na waajiriwa kwenda kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii…”– Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment