Mambo mengine manne aliyoyasema Rais Kikwete ambayo huenda hujayasikia popote kuhusu ugonjwa alioumwa
Henda uliwahi kusikia kitu tofauti kuhusu ugonjwa aliokuwa anaumwa Rais Kikwete, jana Novemba 29 baada ya kuwasili Tz akitokea Marekani, alichokisema hiki hapa;
“…
Operation imekwenda salama na madaktari wamefanikiwa kuyatoa maradhi
yaliyokuwepo mwilini mwangu, yalikuwepo kwenye tezi dume… Sio maradhi ya
busha… Akaja Proffesor mmoja akasema jawabu lake ni tufanye operation
tu, afya yako ni nzuri ukiondoa hiyo utaishi miaka 30 inategemea umri
wako Mwenyezi Mungu amekuandikia miaka mingapi…“– Rais Kikwete.
Nikasema
kama nina miaka 30 huko mbele si haba lakini nitakuwa mzee mno nitakuwa
nina miaka 94, au 95 huko nadhani sitakuwa na manufaa sana.. naweza
kugeuka kuwa mzigo na matatizo kwa watoto na wajukuu mwishoni wakasema
huyu babu hafi…”– Rais Kikwete.
Baada ya kulifahamisha Baraza la Mawaziri kwamba anaumwa, hali ilikuwa hivi;
“…Mheshimiwa Magufuli akaniambia Rais haagizwi lakini hivi kuna ubaya ukiambiwa kwamba Rais Baraza la Mawaziri linakuagiza kwamba usiseme?…
Ni mmoja tu aliyekuwa ananiunga mkono nadhani mama Kabaka tu ndiyo
alikuwa ananiuliza kwamba kwani kuna ubaya gani wa kusema, wengine wote
wakasema wee nyamaza… Hakuna kusema… ” — Rais Kikwete.
Utaratibu ambao umezoeleka mtu
anapofanyiwa operation ni wa kuchomwa sindano ya nusu kaputi, unadhani
Rais Kikwete alifanyiwa hivyo pia wakati wa kufanyiwa upasuaji huo?
“… Wametia
ganzi tu ile sehemu ya chini wanayotaka kufanya operation, wakaniambia
unajua wewe Rais hatuwezi tukafanya uende ile kabisa nusu kaputi ulale
usingizi, unaweza usiamke ikawa taabu… Nilipotoka pale naangalia eeh..!
wameweka vyuma kabisa…“– Rais Kikwete.
Kidonda
kile kimepona wametoa nyuzi lakini walichosema ni kwamba huku ndani
wamekuchana sana kwa hiyo usidanganyike na unachokiona hapa juu kwamba
pameziba lakini huko ndani bado mchakato unaendelea.. Wamesema mpaka
miezi mitatu ndiyo kutakuwa kuna hakika…”
Hiki ndicho alichokisema kwa wale waliokuwa wakimuombea na waliokuwa wakimtumia ujumbe wa kumtakia heri na apone haraka;
Nitoe
shukrani nyingi kwa Watanzania wote, walioniombea dua nipone.. Viongozi
wa Dini na Madhehebu yote nimepata salamu zenu misikitini na makanisani
mmekuwa mkiniombea nawashukuruni sana, nimepona… Mungu amesikia dua zenu
na maombi yenu…”– Rais Kikwete.
Wako
walionitumia sms kwenye simu zangu mpaka zikawa zimezidiwa mpaka
tukafungua line maalum sasa.. Ile simu ilikuwa na message zaidi ya elfu
tano, zimekuja mle watu wengi wakiwa wananiombea heri kwa kweli wote hao
nawashukuru sana.. Ukipata sms zile ni kama vile watu wamekuja
kukuangalia wodini pale…”– Rais Kikwete.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote na Kumekucha Blog
No comments:
Post a Comment