Sunday, November 23, 2014

Wataka kukomeshwa uvivu haramu



Kumekucha Blog

Tanga,WIZARA ya Mifugo na Uvuvi Tanga imetakiwa kuongeza doria katika pwani ya bahari ya Hindi  kuzuia vitendo vya uvuvi haramu wa mabomu na utupa  lengo likiwa ni kulinda rasilimali za viumbe hai baharini.

Rai hiyo imetolewa jana na washiriki wa mashindano ya wavuvi wa samaki yaliyodhaminiwa na kiwanda cha Saruji cha Simba Cement (TCCL)  na kusema kuwa samaki wengi wametoweka  kufuatia  kushamiri kwa uvuvi haramu.

 Alisema samaki wengi wamepotea na viumbe hai vya baharini kufa kufuatia uvuvi huo ambao umekuwa ukifanyika nyakati za usiku na hivyo kuitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kulikomesha

“‘Boti yetu imeweza kutembea hadi karibu na pwani ya wavuvi kisiwani Pemba na tumerejea na samaki  mmoja tu kwa kweli ni aibu---tulikuwa na vifaa vya kisasa vya kuvulia” alisema na kuongeza

“Sababu ni kuwa bado vitendo vya uvuvi haramu vipo jambo linaloashiria miaka mitano Tanga haitakuwa na samaki na hivyo ni wajibu ya mamkala kulikomesha” alisema Asif Ganighee

Alisema kipindi cha nyuma Tanga ilikuwa kituo kikuu cha uvuaji wa samaki na kuwavitia wachuuzi wa ndani na nje ya nchi na hivyo kuitaka kurejeshwa kwa hali hiyo na kuwezesha uchumi wa Mkoa na wananchi kupanda.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Mtanga Noour, aliwataka washiriki hao kuwa mabalozi wazuri kwa wavuvi wengine ili kuwaweka pamoja na kuzungumza changamoto zinazowakabili.

Alisema wavuvi wengi wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi  za baharini na nje ya bahari na hivyo kuyataka mashindano hayo kuwa chachu ya kuwashirikisha wengine mwakani.

“Sekta ya uvuvi iko na changamoto nyingi na nadhani hakuna kiwakutanishacho kama hiki cha leo----kwa kweli kama tutakuwa na utaratibu kama huu sekta hii itakuwa ni yenye maendeleo” alisema Mtanga

Alisema kiwanda cha Saruji kimekuwa kikisaidia makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuwa wavuvi bora na wa kisasa.

Aliwashauri kila mmoja kuwa askari wa mwenzake katika kukabiliana na uvuvi haramu wa upigaji wa mabomu na utumiaji wa nyavu aina ya kokoro pamoja na utupa ili kuurejesha Mkoa huo katika uvuvi wake wa asili.

                                                Mwisho


No comments:

Post a Comment