AC Milan na Inter zavunja rekodi ya miaka 60 michuano ya ulaya
Ni Real Madrid pekee, ambao wameshinda ubingwa wa ulaya mara nyingi kuliko AC Milan, wakati miaka 5 iliyopita Inter Milan walitwaa ubingwa huo.
Lakini wakati vigogo viwili vya soka barani ulaya vitakuwa vikiutafuta ubingwa wa ulaya jijini Milan Mei 2016, hakutakuwa na nafasi ya wenyeji wa mji huo kupata uwakilishi kwenye michuano hiyo.
Timu hizo mbili pia hazitopata hata nafasi kushiriki kwenye michuano Midogo ya Europa – hii ni rekodi ya ambayo haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka 60 kwa aidha AC Milan au Inter kushindwa kucheza katika michuano ya ulaya.
Vilabu hivyo vimeshindwa kumaliza katika nafasi 5 za juu za ligi ya Serie A na hivyo kushindwa kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya ulaya.
Inter Milan imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 8, huku AC Milan ikiwa nafasi ya 10.
Kwa habari na matukio ya ukweli na uhakika ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment