Baba amfungia mkewe bafuni kwa miaka mitatu kisa mtoto wa kike…unajua alikua anampa nini?…
Suala la kuchagua jinsia ya watoto ni
makubaliano kati ya wazazi na pia huwahusisha wote wawili, lakini pia
ujio wa mtoto mwenye jinsia yoyote ndani ya familia ni mapenzi na baraka
za Mungu
Mwanaume huyu raia wa India hakupishana
na baadhi ya wanaume wengi ndani ya jamii zetu ambao wamekua na chaguo
lao wenyewe pindi linapokuja suala la kupata mtoto.
Rameshwar Rao aliamua
kumfungia mkewe na mtoto wake wa kike bafuni kwa muda wa miaka mitatu
kisa tu amemzalia mtoto wa kike kinyume na matarajio yake ya kupata
mtoto wa kiume.
Baada ya mkewe Priyanka
kugundua ni mjamzito wa mtoto wa kike alimwambia mumewe ambaye alimtaka
aitoe mimba kwa kuwa alitaka mtoto wa kiume, lakini mkewe alikataa
kuitoa na kuamua kurudi kwa wazazi wake akajifungue.
Alikaa kwa wazazi wake takribani miaka
mitano na kuamua kurudi wakati mtoto akiwa tayari mkubwa baada ya wote
kusameheana, lakini cha kushangaza mwanaume aliamua kuwafungia bafuni
yeye na mtoto wake huku akiwapa maji na wali kwa muda wote.
Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa na
polisi baada ya marafiki wa familia yake kugundua kitendo alichokifanya
kwa mkewe lakini mke wake amewaomba polisi hao kumwachia huru ili
waendelee kuishi pamoja.
Kwa habari matukio na michezo ya uhakika na ukweli usiache kuwa karibu nami hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment