TANGA KUMEKUCHA
Sunday, June 14, 2015
CHANJO YA POLIO PAKISTAN YASHUTUMIWA
Pakistan yatoa onyo gonjwa la Polio
Maafisa wa utawala nchini Pakistan wametoa onyo kwa wazazi watakaokataa kuwapa watoto wao chanjo ya Polio kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Maafisa wa utawala katika jimbo la Baluchistan, wanasema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuenea upya kwa ugonjwa huo hatari na hivyo kuwalazimu kuchukua tahadhari zaidi.
Wazazi wengi wanashuku kuwa chanjo hiyo ni sehemu ya njama ya mataifa ya Magharibi kupunguza idadi ya Waislamu
Kulingana na mpango huo mpya, kila mtoto atalazimika kuwa na cheti cha kuonesha kuwa tayari amepokea chanjo hiyo ya kupooza kabla ya kupokea huduma yeyote kutoka kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kuingia shuleni.
Familia nyingi zinapinga watoto wao kupokea chanjo kufuatia uvumi kuwa ni njama ya mataifa ya magharibi ya kuwahasi watoto wao kwa nia ya kupunguza idadi ya waislamu duniani.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment