Sunday, June 14, 2015

KIMBUNGA CHAUA WATU NA WANYAMA GEORGIA

Watu na Wanyama pori wasombwa Georgia

Mafuriko makubwa yaliyoikumba mji mkuu wa Georgia, Tbilisi punde ,yamesababisha maafa makubwa huku watu 8 wakithibitishwa kufariki.
Yamkini wenyeji wa mji huo wameombwa kukaaa majumbani mwao baada ya wanyama waliohifadhiwa katika hifadhi moja katikati ya mji huo kusombwa na mafuriko.
Wanyama waliotoweka ni pamoja na simba marara simba wa mwituni,dubu na hata mbweha.
Kati ya wale waliouawa watatu walipatikana ndani ya hifadhi hiyo ya wanyama.
.Makundi ya waokoaji yameanza kutembea nyumba hadi nyengine wakitafuta kuwaokoa manusura na kutathmini hasara iliyotokea baada ya mvua kubwa kunyesha.
.Meya wa mji huo Davit Narmania amesema hali ni mbaya mno huku akiwaasa wenyeji wakae majumbani mwao ilikuzuia matukio ya uvamivizi wa wanyama pori.
Afisa katika Ofisi ya meya wa mji huo anakadiria hasara iliyotokea kuwa ni ya kima cha dola milioni kumi

No comments:

Post a Comment