Tangakumekuchablog
Korogwe, MKUU wa
Wilaya ya Korogwe , Hafsa Mtassiwa, amesema atahakikisha miradi yote
iliyozinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Wilayani humo ataisimamia na
kutekelezwa na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano.
Akizungumza wakati wa mbio za Mwenge
Wilayani humo jana kijiji cha Kerenge kata ya Kwashemshi, Mtassiwa alisema yoyote atakaehujumu miradi ya maendeleo
atawajibishwa na kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Alisema jumla ya miradi ya maendeleo
yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 3kwa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe
Vijijini imezinduliwa na kuwataka
wananchi kutoa ushirikiano ili kuweza kupata maendeleo katika maeneo yao.
“Nasema akutoka moyoni yoyote ambaye
atahujumu au kukwamisha mradi wowote uwe wa uzinduzi wa mbio za mwenge au wa
aina tofauti ya maendeleo nitamchukulia hatua za kisheria” alisema na kuongeza
“Serikali imekuwa ikifanya jitihada
za kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini utaona kunatokea mtu au kikundi cha
watu kwa makusudi anahujumu----hili binafsi sitakubaliana nalo” alisema
Akitoa ujumbe wa mwenge wa Uhuru,
kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Juma Khatib Chumu, amewataka wananchi kuchagua
viongozi wenye uwezo wa kuongoza nchi na kuacha kuchagua kwa ushabiki wa
kisiasa.
Alisema kipindi hiki cha kuwapata
wagombea wa nafasi za Urais kutazuka watu na kutoa ahadi nyingi ili kuweza
kupata wafuasi na hivyo kuwataka kuwa makini na watu hao.
“Ndugu zangu tunakaribia uchaguzi
mkuu wa kumpata Rais wabunge na madiwani---watakuja watu na kutoa ahadi
kemekem---zipimeni kisha mupambanue na kuchukua uamuzi” alisema Chumu
Amewataka kuwa makini na wagombea na
kuhakikisha wanachagua kiongozi bora na mwenye uwezo wa kuongoza na mwenye uchu
wa kuwaleta maendeleo wananchi wake.
Mwisho
No comments:
Post a Comment