Saturday, June 13, 2015

UJERUMANI YADAI WAHAMIAJI NI MUHIMU KIUCHUMI

Ujerumani:Wahamiaji ni Muhimu

Maafisa nchini Ujerumani wamesema kuwa idadi inayozidi kuongezeka ya wakimbizi wanaowasili kutoka Bara la Afrika  kama Syria watasaidia kujaza pengo la ukosefu wa wataalamu.
Mwenyekiti shirika la ajira nchini Ujerumani aliliambia gazeti moja kuwa watu wanaokimbia Syria, wengine wameelimika na hivyo wanakaribishwa nchini Ujerumani.
Wakimbizi 350,000 watarajiwa kutafuta ajira nchini Ujerumani mwaka huu.
Ujerumani hupokea maombi mengi ya hifadhi kuliko nchi yoyote katika muungano wa Ulaya na idadi hiyo inazidi kuongezeka.

No comments:

Post a Comment