Sunday, June 14, 2015

ICC YAITAKA AFRIKA KUSINI KUMKAMATA OMAR EL BASHIIR

ICC yaitaka A. Kusini kumkamata Bashir

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeitaka Afrika Kusini kumkamata Rais wa Sudan Omar Al-Bashir ambaye anaripotiwa kusafiri kwenda nchini humo kuhudhuria mkutano wa Muungano wa nchi za Afrika ambao unaanza leo Jumapili.
Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado ziko. Anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.
Kama mwanachama cha ICC, Afrika Kusini imetakiwa  kumkamata Bashir ikiwa atasafiri kwenda nchin humo . Lakini Muungano wa Afrika umekataa kushirikiana na mahakama hiyo ya kimataifa ukisema kuwa ICC inawaonea viongozi wa Afrika.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment