MWANANCHI
Makada wa CCM waliotangaza nia au
kuchukua fomu za kuomba kupitishwa na chama hicho kuwania urais,
wameeleza jinsi rushwa, ufisadi na udhaifu katika ukusanyaji kodi huku
wakijinadi kuwa wao ndiyo wataondoa uovu huo iwapo watapitishwa kushika
nafasi hiyo ya juu kisiasa.
Lakini hakuna hata mmoja aliyeiponda
Serikali kwa kushindwa kudhibiti rushwa, ambayo baadhi walishasema kuwa
imekithiri hata kwenye chama hicho tawala, huku mmoja akisema kuwa iwapo
CCM itampitisha mlarushwa, atajiondoa.
Kati ya waliotangaza nia na kuchukua
fomu, makada 11 ni mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne wakiwamo
mawaziri waandamizi walioshika nafasi za juu na waliofanya kazi katika
awamu zote nne.
Pia wamo makada waliokuwamo kwenye
Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Nne, lakini wakaondoka kwa
sababu tofauti, huku kundi jingine likihusisha watendaji wakuu wa zamani
wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Lakini bado tatizo hilo la rushwa
limekuwa likitumiwa na makada hao wa CCM wanaowania urais wakati
wakijinadi kwa wanachama wao kwamba watafumua mfumo uliopo, kusuka upya
sheria na kuimarisha taasisi za fedha ili watuhumiwa wakubwa wa rushwa
wafikishwe kortini na kufungwa, badala ya kuwakamata walarushwa
wadogowadogo pekee.
Kwa mfano, akitangaza nia ya kuwania urais kijijini kwao Butiama, Charles Makongoro
ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema
anaomba kibali cha kuisaidia CCM ikomeshe rushwa, na atakapoingia
madarakani, ili asiwaangushe Watanzania, anahitaji chama imara kisicho
na shaka kama ilivyo sasa.
“Kosa la Rais Jakaya Kikwete ni kuwapenda sana marafiki zake. Kwa bahati mbaya, baadhi ya marafiki zake hao ni vibaka,” alisema Makongoro ambaye ni mbunge wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe
aliwaambia wafuasi wake mkoani Lindi kwamba ili kutekeleza utawala
bora, hawezi kukaa kimya kuona rushwa, ubadhirifu, ufisadi vikichukua
nafasi katika utawala wake.
“Ninawatumia
salamu mapema, sitakuwa na kigugumizi kwa wanaotesa Watanzania.
Nitahakikisha Watanzania wanachukia rushwa na kutakuwa na sheria kali
dhidi ya mtoa na mpokeaji rushwa. Kama ni watumishi wa umma, watakwenda
na maji…,”
Ahadi ya kukomesha rushwa pia ilitolewa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
aliyesema kwamba anataka kulifanyia Taifa mambo matano, ikiwa ni pamoja
na kutenganisha biashara na siasa na kusimamia maadili ya viongozi wa
umma.
“Ili kukomesha tatizo la rushwa, hatuna budi kutunga sheria itakayotenganisha biashara na uongozi,” alisema Sitta kwenye Ikulu ya Wanyanyembe iliyopo Itetemia, Tabora.
MWANANCHI
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasimama kifua mbele kupambana na rushwa kwa kuwa aliwahi kuikataa rushwa ya Dola 70,000 (sawa na Sh140,000) milioni).
Sitta alisema kuna baadhi ya watia nia
wanaopita wakisema kuwa wakiwa marais watapambana na rushwa wakati
ukiwatazama macho yao yanaonyesha ni wala rushwa.
“Nilitumwa
Canada kutafuta ndege tatu, jioni moja tukiwa Canada tunajiandaa
kuondoka, akaja mkurugenzi wa masoko wa kampuni tuliyonunua ndege,
akaniambia waziri tuna kautaratibu hapa ukifanikisha ndege zetu
zikanunuliwa tunatoa bakshishi ya Dola 70,000 utataka hizi hela
tuzipeleke benki gani,” alisema Sitta akimnukuu ofisa huyo wa masoko.
“Watazameni
hawa watu… mtu kawa waziri mwaka mmoja leo anataka urais, halafu
anasema atapambana na rushwa…utapambana na rushwa wapi wakati hata
hujapita kwenye mitego ya rushwa. Watazameni kwa makini, mtawajua tu kwa
macho, kwani macho yao yamekaa kijanjajanja kweli,” alisema.
Aliendelea, “Kwa kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu huo ni mtego wa
shetani, nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho, nikawasiliana na
wakubwa zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa ikasomeshe marubani
wa ndege.”
Sitta aliwataka wananchi hao kuwatazama
kwa makini watangaza nia hao, na kuwauliza iwapo tayari walishawahi
kupambanishwa na rushwa.
Wakazi wa Kigoma wametakiwa kuwa makini
na kauli za baadhi ya viongozi wa Serikali wanaojinadi kwa kusema
wanawapenda Watanzania maskini, lakini mioyoni mwao hawana huruma.
Akiwa katika ofisi ya CCM mkoa, Katibu
wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Nohoji Kubaji alimkabidhi Lowassa fomu 45
za wana CCM waliomdhamini.
“Wapo
viongozi, wanajifanya wanawapenda na kuwajali watu masikini, lakini wao
wenyewe unawakuta ni matajiri, hawa jamaa ni waongo sana hawa,”.
Lowassa aliwataka wakazi Kigoma kumuombea ili dua na sala zao ziweze kumsaidia afikie malengo aliyojiwekea. “Nina
dhamira ya kuwatumikia, lakini lazima mniombee sana dua na sala ili
mambo yangu yaende vizuri hatimaye nishinde kuwa Rais wa Tanzania. Mimi
nachukia sana umaskini, kwa hiyo lazima tuwe kama Malaysia ambayo
kiongozi wake alipambana kuhakikisha wananchi wanaondokana na umaskini,”.
MWANANCHI
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
ameitaka CCM kujiandaa kisaikolojia kukabidhi madaraka kwa chama chake
baada ya Oktoba, akisema katika chama chake hakutakuwa na neno “kushindwa”.
Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, aliwataka vijana popote walipo kujiandikisha
kwa ajili ya uchaguzi ili kujitayarisha na ushindi aliouita mkubwa.
“Hakuna
kushindwa CUF, kwa hivyo mawazo yenu yawe na kushinda tu. Vijana,
hakuna kukaa ukasema ushamaliza kupiga kura, unakwenda kwako unasubiri
ushindi. Hakuna hilo mwaka huu, lazima mjitahidi kulinda ushindi wenu,” Maalim Seif.
Katibu huyo wa CUF alisema wananchi wa
Pemba walioko Arusha, Mwanza na sehemu nyingine warudi kujiandikisha
kwenye Daftari la Wapigakura na kuwataka kutoacha fursa hiyo ambayo ni
haki yao ya kidemokrasia.
Akitilia mkazo suala hilo, aliyekuwa waziri wa SMZ, Mansoor Yussuf Himid alimtaka Maalim Seif baada ya kupiga kura yake kurudi nyumbani na kuwaachia vijana kumkabidhi ushindi wa chama hicho.
Mansoor alisema hatima ya ushindi wa
Zanzibar ipo mikononi mwa vijana, hivyo wanapaswa kuhakikisha ushindi wa
Zanzibar unapatikana katika ya mikono yao.
Akihutubia mkutano huo, Mwanasiasa Hassan Nassor Moyo
alisema kazi ya Maalim Seif na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid
Karume kuleta umoja wa kitaifa si jambo jipya kwa kuwa lilianzia kwa
Mzee Karume ambaye alitunga sheria kuondosha ubaguzi na kuwaweka
wananchi wote wa Zanzibar kuwa kitu kimoja.
Katika hotuba yake ya takriban saa moja
iliyorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV, Maalim
Seif alisema Maalim Seif alisisitiza nia yake ya kuifanya Zanzibar kuwa
na mamlaka kamili ili iondokane na adhabu ambazo siyo stahiki kwake.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete
ametokwa na machozi wakati akisikiliza wimbo ya masikitiko ya watoto
wenye ulemavu wa ngozi (albino), na akaeleza kuwa ni upumbavu kuamini
kuwa viungo vyao vinaleta utajiri.
Rais Kikwete alisema mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayoendelea nchini yanamsononesha na kulitia doa Taifa.
Rais Kikwete alisema wimbo wa watoto
wenye albino kutoka Tanga, ulivyoanza alianza kuhisi angetokwa machozi
na baadaye alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi.
“Hawa
watoto wameimba mambo ambayo yamenigusa sana, na tumepokea kilio chenu
kwa umuhimu mkubwa na ninaahidi tutashirikiana kuyashughulikia matatizo
yenu,” alisema.
Alisema suala la matibabu ya albino ni
jambo ambalo linashughulikiwa, ili kuhakikisha vifaa tiba ambavyo
vinahitajika hasa kutibu magonjwa ya ngozi vinapatikana na kuwawezesha
kupata matibabu bure.
Akizungumzia hatua za Serikali, Rais Kikwete alimpa nafasi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe kueleza hatua zilizofikiwa katika kuunda kamati ya kitaifa ya kuishauri Serikali.
Waziri Chikawe alieleza kuwa tayari
wizara yake, imekamilisha mchakato wa kuunda kamati hiyo, ambayo itakuwa
na wajumbe 15, watano kutoka chama cha wenye albino, watano chama cha
waganga wa jadi na watano kutoka serikalini.
Awali Mwakilishi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNICEF) nchini, Zulmira Rodrigues
aliiomba Serikali kuwaondoa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)
waliowekwa katika vituo maalumu, kwa kuwa kitendo hicho kinawanyanyapaa.
Akizungumza katika mkutano uliokuwa wa
kuelezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu albino
jijini hapa jana, Rodrigues alisema vituo hivyo vinaweza kutumika kwa
ajili ya kuwahifadhi albino kwa muda mfupi na si kuvifanya suluhisho la
kudumu litakalowapa ulinzi.
MTANZANIA
Baba mmoja anayetajwa kwa jina la Maneno Kasugu anadaiwa kumchinja hadi kufa mtoto wake mwenye umri wa mwaka .
Kasugu ambaye anaelezwa kuwa ni mlinzi,
anadaiwa kutekeleza kitendo hicho cha kinyama jana saa 4 asubuhi eneo la
Mabibo Loyola Jijini Dar es salaam baada ya kumteka mtoto wake huyo
aliyekuwa akiishi na bibi yake mzaa mama.
Bibi huyo Mwanaidi Hassan
ambaye alikua akishi na mjuu wake huyo hadi mauti inamkuta alisema
alieleza sababu mbili ambazo anadhani huemda zimechangia kifo cha mjuu
wake.
Alidai Kasugu na mkewe walikua na ugomvi
na pia kushindwa kutumia kiasi cha shilingi 50,000 alizotoka mkwe wake
huyo baada ya kumteka mtoto.
Kwa mujibu wa bibi huyo Kasugu alifika nyumbani hapo saa mbili asubuhi na kisha kumchukua mtoto bila taarifa.
“Mimi nilikua bado nimelala, mama wa
mtoto alikua chumbani kwake na mtoto alikua anacheza, alipofika
akamchukua mtoto na kuandoka”.
Anasema baada ya muda kupita bila mtoto
kuonekana ndipo mama wa mtoto alipoamua kumpigia Kasugu simu kutaka
kufahamu na kutaka atumiwe 50,000 ili awaeleze mtoto alipo na tofauti na
hapo asingeonekana.
Baada ya muda watu walidai kukuta mwili
wa mtoto aliyechinjwa ukiwa nyuma ya shule ya Loyola na ndipo walipotoa
taarifa kituo cha polisi cha urafiki ambao wlaifika na kuuchua mwili wa
mtoto huyo.
NYAKATI
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
amewataka Watanzania kumuombea sana kwa Mungu ili chama chake kiweze
kumchagua kuwa Rais kwani amejiandaa kuipeleka nchi katika mchakamchaka
wa maendeleo.
Pia amesema akifanikiwa kuwa Rais atamwaga milioni 500 kwa kila kata kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo.
Alisema wachimbaji wadogowado wa madini watapewa mikopo ili kuwawezesha kujiimarisha katika shughuli zao za uchimbaji wa madini.
Alisema yeye anawapenda sana Watanzania
hali iliyomfanya achukue uamuzi wa kugombea kutokana na kuguswa na hali
ya umaskini wa wananchi wenzake.
Alisema ili kuwakomboa wananchi kama watampa ridhaa ya kuwaongoza, ataifikisha Tanzania pazuri.
Uchambuzi huu umeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinmaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha na wanaojiendeleza kielimu. simu 0715 772746
No comments:
Post a Comment