Thursday, June 4, 2015

KASHFA YA RUSHWA FIFA

Kashfa ya rushwa FIFA, mmoja amekiri kupokea, mwingine aapa kufichua ufisadi..!!

chukk
Wakati sakata kuhusu tuhuma za rushwa likiendelea kuliandama Shirikisho la soka duniani FIFA huku baadhi ya Maofisa wake wakishikiliwa na Rais Blatter kujiuzulu, kuna habari nyingine inayohusiana na kashfa hiyo.
Taarifa iliyopokelewa na Wizara ya sheria ya Marekani inayoelezea jinsi afisa wa zamani wa FIFA Chuck Blazer kukiri yeye na viongozi wenzake kupokea rushwa ili kuichagua Afrika kusini kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la duniani mwaka 2010.
wanaer
Aliyekuwa makamu wa Rais wa FIFA Jack Warner
Mbali na Blazer pia aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner amesema kwamba atafichua kila anachojua kuhusu ufisadi ndani ya shirikisho hilo.
Taarifa hiyo imeweka wazi mtandao wa malipo uliofanywa ndani ya Shirikisho hilo wakati wa uchunguzi uliofanywa na wapelelezi wa Marakeni FBI
Kitendo cha Afisa huyo wa zamani wa FIFA, Chuck Blazer kukiri kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa inayowahusu FIFA.
Mmarekani huyo kwenye taarifa hiyo inadai alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka mipango ya kupokea rushwa katika tukio jingine la fainali la kombe la dunia 1998.
Marekani imefungua kesi ya rushwa inayowakabili maafisa wa FIFA..kesi inayohusu kupokea rushwa ya dola milioni 150 jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.
Kwa habari na matukio ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment