Thursday, June 4, 2015

WATU 90 WAFARIKI BAADA YA KITUO CHA MAFUTA KURIPUKA

Baada ya ajali ya lori la mafuta Nigeria, hii nyingine ni kituo cha mafuta kuwaka moto Ghana

mooo
Mapema wiki hii tangakumekuchablog iliandika stori ya ajali ya lori la mafuta kuua zaidi ya watu 90 Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na kugonga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo cha abiria.
station
Muonekano wa kituo cha mafuta baada ya kulipuka
Lakini leo Ghana nayo imeingia kwenye headlines baada ya kituo cha mafuta kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi hiyo Accra.
Mlipuko huo umetokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo mengi ya mji huo ambapo pia imewaacha watu wengi bila makazi huku sehemu kubwa ya mji ikiwa gizani kutokana na kukatika kwa umeme.
mtoto
Mwili wa mtoto ukiokotwa katika eneo la kituo hicho
Idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka kwani watu wengi wamepoteza maisha baada ya kuwepo kituoni hapo wakijikinga na mafuriko yaliyotokea na huenda idadi ikaongezeka kutokana na baadhi ya miili kuwa bado haijapatikana.
Kwa habari, matukio mengi moto moto,. ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment