Monday, June 15, 2015

KASISI ANYIMWA KAZI KWA KWENDA KINYUME NA KANISA

Kasisi basha aishtaki kanisa kumbagua

Kasisi mmoja ambaye alinyimwa leseni ya kufanya kazi kama mhudumu katika zahanati ya afya kwa misingi ya kuwa katika ndoa ya jinsia moja ameishtaki kanisa kwa kumbagua.
Jeremy Pemberton alikuwa amewasilisha pendekezo la kutaka kuhudumu kama Kasisi katika kanisa lililoko ndani ya hospitali.
 Pemberton anadai kuwa maombi yake yalipingwa  na kaimu askofu wa Southwell na Nottingham nchini Uingereza.
Rt Revd Richard Inwood alimkashifu  Pemberton kuwa katika ndoa na mwanaume mwenza ambaye ni kinyume na mafundisho ya kanisa la Church of England.
Tume inayosimamia utoaji kazi nchini Uingereza inatazamia kuanza kuisikiza kesi hiyo leo..
Askofu Inwood, alimnyima kazi kasisi Pemberton, na kisha akaiandikia barua bodi inayosimamia hospitali hiyo ya Sherwood Forest akiwashauri wasimpe kazi kasisi Pemberton.

No comments:

Post a Comment