Monday, June 15, 2015

OMAR AL BAASHIR AREJEA KHATOOM LICHA YA KITISHO CHA KUKAMATWA

Bashir amewasili mjini Khartoum Sudan

Rais Omar al Bashir wa Sudan amewasili mjini Khartoum Sudan akitokea Afrika Kusini.
Rais Bashir amekariri wakuwa hana hatia yeyote wala hajui kwanini mahakama ya kimatiafa ya ICC inasisitiza kumchafulia jina.
Shirika la habari ya AFP limemnukuu rais Bashir akifoka ''Allah Akbar'' aliposhuka kutoka kwa ndege iliyombeba.
Aidha aliinua mkongojo wake juu na kushabikiwa na wafuasi wake.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Sudan Ibrahim Ghandour aliwaambia waandishi wa habari kuwa Serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imemkariri Rais Bashir kuwa kuwepo kwake mjini Johannesburg ilikuwa ni tukio la kushabikiwa na lenye heshima kubwa kwa hivyo hakukuwa na uwezekano wowowte  kukamatwa.
Awali kuondoka kwake nchini Afrika Kusini kulikumbwa na hatihati, baada ya mahakama moja kuamuru rais huyo asiondoke nchini humo hadi mahakama hiyo itakaposikiza kesi na kuamua iwapo atakamatwa na kupelekwe mjini the Hague Uholanzi au la.
Awali Mwandishi wa BBC aliyeko Afrika Kusini Nomsa Maseko, alisema kuwa ndege ya rais al Bashir ilijazwa mafuta jana usiku na kuwekwa mstari wa mbele tayari kabisa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment