Idadi kubwa ya ndovu yatoweka Tanzania
Wanaharakati
wa wanyamapori wameelezea hali ya kutoweka kwa idadi ya ndovu kwa
asilimia sitini nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita kama janga.
Kwa mujubu wa kikundi kinachofuatilia maisha ya wanyamapori, TRAFFIC, linasema idadi hiyo inaashiria kiwango halisi cha uwindaji haramu.Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Lazaro Nyalandu, amesema kuwa tatizo hilo lipo kwa kiwango tofauti nchini humo, akitoa mfano kuwa eneo la Serengeti idadi yao inaongezeka .
Amesema mamia ya walinzi wa wanyamapori wamekodiwa kukabiliana na uwindaji haramu
No comments:
Post a Comment